Posts

Showing posts from January, 2026

ALIANZA UJAMBAZI AKIWA NA MIAKA KUMI, JAMBAZI SUGU KUTOKA INDIA

 Swahili Prime Ent Anaitwa Koose Munisamy Veerappan raia wa India aliyezaliwa 18 January 1952. Unaambiwa India waliwahi kutokea majambazi sugu na kudhibitiwa, lakini huyu ndio alikuwa kiboko. Alifanya shughuli za uhalifu kwa miaka 42 kabla ya kudhibitiwa na kuuwawa Oktoba 18, 2004 akiwa na miaka 52. Veerappan ni nani? Kila kitu kumhusu yeye kipo hapa Veerappan aliyezaliwa huko Coimbatore, India alianza kazi yake ya uhalifu tangu akiwa na umri wa miaka 10 kwa msaada wa mjomba wake Saalvai Gounder, walikuwa wanauwa tembo na kuvuna pembe za ndovu na kuuza kimagendo huku makazi yao makubwa yakiwa misituni, na baada ya muda alitengana na mjomba wake na kuanza kujitegemea. Rekodi inaonyesha kuwa katika wakati wake wote kama muhalifu 1962–2004 ameuwa zaidi ta Tembo 900, lakini ukweli ni kwamba ameuwa kati ya tembo 2000 - 3000, ameuwa watu 184 wakiwepo askari 97 na maafisa wa misituni huku akiigharimu serikali ya India zaidi ya $ 330 milioni kufanikisha kumtia nguvuni (zaidi ya TZS Bilion ...

SIMBA WALIOKWAMISHA UJENZI WA RELI KWA MWAKA MZIMA

 Swahili Prime Ent Kwa Mujibu wa Taarifa ya Uchunguzi, Mwaka 1898 Simba Wawili Wakali Walidaiwa Kutumwa Kwa Makusudi ili Wakawauwe Wafanyakazi Waliokuwa Wanajenga Reli ya Kenya - Uganda na Kukwamisha Ujenzi Huo kwa Karibia Mwaka Mzima. Simba Hao Wanadaiwa Kuwala Wafanyakazi 140. Katikati ya machi 1898 usiku, wafanyakazi katika mradi wa reli ya Uganda, ambayo inaunganisha na Kenya, walishambuliwa na simba wawili na kuibuka mauaji ya kutisha zaidi ya mnyama kuwashambulia binadamu katika historia. Iweje itajwe kuwa simba walitumwa? Madhara na mwisho wake ulikuwaje?  Inaelezwa kuwa Machi 1898 simba wawili waliwavamia wafanyikazi usiku wa manane katika kambi yao na kusababisha vifo vya wafanyikazi 140 wa Kiafrika na Wahindi, na iliainishwa kama mauaji mabaya zaidi kufanywa na mnyama dhidi ya wanadamu katika historia. Lakini nyuma ya pazia inaelezwa kuwa sababu ya mauaji hayo ni simba hao kutumwa, kusogezwa makusudi karibu na mradi ili wawashambulie wafanyakazi kwasababu wahusika wa...

MFUNGWA HATARI ALIYETOROKA GEREZANI KWA KUTUMIA UZI!

 Swahili Prime Ent: Mfungwa Robert Dale Shepard Raia wa US Aliyetumia Kamba za Kusafishia Meno Kutoroka Katika Gereza la South Central Regional Jail Virginia kwa Kukwea Ukuta wa Futi 18 Mwaka 1994. Alifuma Kamba ya Futi 20. June 29, 1994 mfungwa Robert Dale Shepard (34) aliyekuwa anatumikia kifungo katika gereza moja mashariki mwa Virginia US, alifanikiwa kutoroka gerezani kwa kupanda ukuta akitumia kamba nyembamba ya kusafishia meno. Inaelezwa kuwa baada ya kutoroka alitumia siku 41 kuishi msituni, akiishi kwa matunda na kuoga kwenye mito, hadi alipokamatwa tena akiwa amenyooshewa bunduki na askari baada ya kudaiwa kuiba duka la dawa karibu na mji wake wa Parkersburg. Shepard alikuwa akikusanya kamba ndogo kwa miezi mingi zilizokuwa zinagawiwa kwa wafungwa ili kusafishia meno gerezani hapo, akaunganisha na kufuma kamba moja ndefu na imara iliyomsaidia kutoroka kupitia ukuta wa gereza wa futi 18. Katika mahojiano yake baada ya kukamatwa Shepard alisema kua kabla ya jaribio lake ku...

Anaitwa Chris McCandless Raia wa California US. Mwaka 1992 Akiwa na Miaka 24 Aliamua Kuingia Porini, Mbali ili Akaishi Maisha ya Asili, Maisha Kama ya Wanyama kwa Miezi 3 Kisha Arudi Nyumbani. Miezi Mitatu Baadaye Mwili Wake Ulipatikana Umeoza Porini. Inaelezwa Alikufa kwa Njaa.

Majina yake halisi anaitwa Christopher Johnson McCandless mzaliwa wa California US. Kwa hiyari yake mwenyewe katikati ya mwaka 1992 akiwa na miaka 24 aliamua kutoka nyumbani kwake na kuingia porini mbali huko Alaska ili kujipatia uzoefu wa maisha mapya ya asili yasiyowategemea binadamu wengine. Chriss Aliingia porini kupata uzoefu wa kuishi maisha kama mnyama wa porini, alipanga kuishi huko kwa miezi mitatu na kurejea nyumbani huku akibeba notebook ya kuandika vidokezo pamoja na camera ndogo. Taarifa zinasema kuwa Chris alikufa miezi mitatu baadae Agosti 18, 1992, ikiwa ni siku ya 112 baada ya kutembea porini. Mwili wake ulipatikana siku 19 baadaye pamoja na notebook yake na camera. Kuna uwezekano mkubwa kwamba Chriss alikufa kutokana na njaa na utapiamlo. Chris alitaka kuishi kiasili akiwa porini kwa miezi michache. Kweli baada ya miezi mitatu huko porini alianza safari ya kurudi nyumbani lakini alipofika mto Teklanika alikuta mto umejaa maji mengi kiasi cha kushindwa kuvuka. Kati...

SIRO NZITO:JINSI FAMILIA YA GLAZER ILIVYOICHUKUA MANCHESTER UNITED KIMAFIA NA KUIINGIZA KWENYE MADENI MAKUBWA!

Swahili Prime Ent Leo tunaitazama historia ya kushtua ya jinsi bilionea Malcolm Glazer alivyofanikisha ununuzi wa Manchester United kati ya mwaka 2003 na 2005. Huu ulikuwa ununuzi uliogubikwa na malalamiko mengi ambayo hadi leo yamesababisha vuguvugu la Glazers Out. Hatua kwa Hatua ya Ununuzi: 1. Mwanzo Mdogo (Machi 2003): Malcolm Glazer alianza kwa kununua hisa ndogo tu ya 2.9% kwa takriban pauni milioni 9 (£9M). Wakati huo, United ilikuwa kampuni iliyoorodheshwa kwenye soko la hisa. 2. Ujanja wa Soko la Hisa:Kwa kipindi cha miaka miwili, Glazer aliendelea kununua hisa kidogo kidogo sokoni hadi akafikia kiwango cha kuanza kuidhibiti klabu. 3. Mapinduzi ya Mwaka 2005: Mwezi Mei 2005, familia ya Glazer ilikamilisha ununuzi wa karibu 98% ya klabu kwa thamani ya pauni milioni 790 (£790M). Kwanini Mashabiki Walikasirika? (Leveraged Buyout): Hapa ndipo penye siri ya madeni ya United. Glazer hakutumia pesa yake yote mfukoni. Badala yake: Alikopa kiasi kikubwa cha fedha (takriban pauni milion...

MWANAMKE ALIYETABIRI MAMBO YANAYOTIMIA HADI WAKATI HUU

 Swahili Prime Ent: Moja ya Utabiri Aliouacha Baba Vanga Raia wa Bulgaria, Mmoja wa Watabiri Maarufu Kutokea Alisema Kuwa Kuanzia Mwaka 2023 Itakua ni Kawaida tuu kwa Mwanake Kwenda Maabara Kupandikizwa Mtoto na Baadaye Kuzaa. Alifariki Mwaka 1996 Akiacha Tabiri Zaidi ya 100, na Nyingizo Zinatimia.   Baba Vanga ni Nani? Baba Vanga alikuwa mwanamke kipofu ambaye aliacha ubashiri kwa kila mwaka hadi mwaka 5079. Alizaliwa Vangelia Pandeva Dimitrova Bulgaria.  Alipokuwa na umri wa miaka 12, dhoruba ilimpiga na kumfanya apotee katika machafuko hayo na kupoteza uwezo wake wa kuona. Alipatikana siku chache baadaye akiwa kipofu. Baba Vanga alidai kuwa alipata maono yake ya kwanza katika siku alizopotea na kimbunga hicho, na baadaye alisema uwezo wake wa kuona umebadilishwa, badala ya kuona kawada yeye anaweza kuona siku zijazo. Alifariki mwaka 1996 (85). BAADHI YA UTABIRI WAKE ULIOTIMIA. 1️⃣Mwaka 1989 Vanga alisema: "Waamerika wataanguka baada ya kushambuliwa na ndege w...

Erna Petri Aliwakamata Wayahudi Sita Waliotoroka Kwenye Treni Iliyokuwa Inawapeleka Kwenye Kambi ya Kifo Germany, Akawalisha Vizuri na Kuwalaza Pazuri kwa Wiki Zima, Kisha Akawapeleka Msituni na Kuwachinja. Je Erna Petri ni Nani?

 Swahili Prime Ent Wakati wa vita ya pili ya dunia mwaka 1939-1945, huko Ujerumani chini ya Adolf Hitler Wayahudi walikuwa wanauliwa kama kuku kutokana na chuki kubwa ya kiongozi huyo wa kinazi dhidi yao. Kufuatia chuki hiyo kulitengenezwa kambi mbalimbali za mateso na mauwaji ya kinyama dhidi ya wayahudi, walikuwa wakikamatwa na kusafirishwa kwa treni mpaka ziliko kambi hizo na kisha kupata mateso na kuuwawa Horst Petri alikuwa ni mmoja wa maofisa wa ngazi ya juu na wa karibu wa Hitler, hivyo kuwa ni mmoja wa watekelezaji wakubwa wa mateso na mauwaji dhidi ya wayahudi. Mwaka 1943 wakati maelfu ya wayahudi wakiwa njiani kupitia usafiri wa treni wakipelekwa katika moja ya kambi ya mateso, kuna wayahudi 6 walifanikiwa kutoroka na kujiokoa katika safari hiyo ya kifo, lakini kwa bahati mbaya wakakamatwa na Erna Petri ambaye ni mke wa Hosrt Petri. Historia imeandika kuwa Erna aliwapatia huduma nzuri kwa karibia wiki zima, akiwapa mahala pazuri pa kulala pamoja na chakula kizuri, lakini ...

JIWE LILILOTABIRIWA KUIPIGA DUNIA NA KUUA KILA KIUMBE!

 Swahili Prime Ent: Mwaka 1907 Dunia Iliingia Kwenye Hofu Kubwa Baada ya Kutangazwa Kuwa Mwaka 1910 Jiwe Kubwa Lenye Gesi Kali Litaonekana Angani, Litapasuka na Gesi Yake Itauwa Kila Kiumbe Kilichopo Duniani. Ni Kweli Mwaka 1910 Jiwe Hilo Lilionekana na Watu Wengi Kufa kwa Mshtuko Akiwemo Mfalme wa Uingereza.  Kutokana na kuanza kukua kwa teknolojia, wataalamu wengi wa dunia walianza kutumia vyombo vya kitaalamu kugundua nini kinaweza kutokea mbeleni. katika upande wa hali ya hewa na kwingineko, na hapo ndipo mwanaanga maarufu wa Ufaransa Camille Flammarion alipotangaza hatari kubwa inayotarajia kuikumbwa dunia mwaka huo 1910. Mwaka 1907 Flammarion alitangaza kuwa kuna jiwe kubwa mfano wa nyota lenye gesi yenye sumu hatari ya cyanogen litapasuka angani mwaka 1910 na gesi yote itasambaa duniani na kuondoa maisha ya kila kiumbe kilichopo ndani ya dunia. Watu waliuamini mwisho huo wa dunia kwani ni kweli jiwe hilo kubwa linaloitwa Halley's Comet kitaalamu lilikuwa likitokea tang...

MWAMBA ALIKUWA HAFANYI MAZOEZI LAKINI ANATUPIA KILA MECHI

Unasema Wachezaji Wengi wa Soka wa Sasa ni Watukutu? Karibu Nikusimulie Kisa cha Mchezaji Giuseppe Meazza Raia wa Italia. Yeye Alikuwa Hafanyi Mazoezi na Timu Yake Lakini Anatupia Kila Mechi, Anavuta Sigara Hata Kwenye Half Time ya Mechi na Hakuna Anaesema Lolote, San Siro Kuna Jina Lake. Meazza alizaliwa mwaka 1910 huko Italia, alipokuwa mchezaji wa soka alizoea kuvuta sana sigara kiasi kwamba alikuwa anaweza kuvuta sigara wakati wa mapumziko ya mechi mbele ya wachezaji wenzake na kocha wake. Wachezaji walimzoea mchezaji huyo na staili yake. Meazza alikuwa akifanya mazoezi na timu yake ya Inter Milan kwa siku moja tu kwa wiki au asifanye kabisa, lakini kwenye mechi anakupa kila kitu unachotaka uwanjani, wachezaji na mashabiki wa klabu yake ya Inter Milani walimpachika jina la 'The Miracle'. Moja ya matukio ya ajabu ambayo nimesoma kuhusu mchezaji huyo ni katika mechi ya dabi kati ya timu yake ya Inter Milan na AC Milan. Picha linaanza jamaa anammka nyumbani dakika 5 tuu kabla ...

MCHAWI ALIYETENGENEZA KEKI YA MAJIMAJI YA SEX NA DAMU YA HEDHI NA KUWAPA WAUMINI WAKE!

Anaitwa Aleister Crowley Raia wa UK. Anajulikana Kama Baba wa Uchawi. Katika Imani Yake na Waumini Wake Kulikuwa na 'Cake of Light', ni Keki Inayotengenezwa kwa Majimaji ya Sex na Damu ya Hedhi. Alikuwa Anajiona Anazo jinsia Mbili Hivyo Kuwa na Wapenzi wa Kike na Wakiume. Miaka ya mwanzoni mwa 1900 Crowley alikuwa ni mchawi hatari katika dunia, umaarufu wake yeye na imani yake vilisambaa duniani kote. Nchini Algeria kuna sehemu inaitwa Tassili N'Ajjer, kwasasa ni hifadhi ya taifa lakini zamani kabla ya miaka ya 1900 ilikuwa ni sehemu ya kuogopwa mno kuingia kutokana na kuaminika kwamba kuna majini, hakuna yeyote aliyekua amewahi hata kuisogelea. Wakoloni ambao ni Ufaransa waliogopa hata kulisogelea eneo hili la mapango na kuishia kupiga picha kwa juu tuu kwa kutumia ndege, lakini mwaka 1909 mwamba alipopata taarifa za eneo hilo alienda na kuingia mpaka ndani na kutoka, japo wenzake alioongozana nao walipotelea ndani humo. Crowley alizaliwa Oktoba 12, 1875 nchini Uingereza, ...

ALIMCHINJA MKE WAKE NA KUANDIKA HIYO STORY KWENYE KITABU!

 Swahili Prime Ent: Richard Kleinhammer ni Mwandishi wa Vitabu wa Uholanzi, Mwaka 1991 Alimchinja Mke Wake Hannelore na Kisha Kuandika Stori Hiyo Yote ya Mauwaji Katika Kitabu Chake na Kuuza Nakala Zake. Kitabu Kinaitwa 'Jumatano Siku ya Nyama ya Kusaga', Mwaka 2000 Alikamatwa na Kutiwa Gerezani kwa Mauwaji Hayo ya Mkewe. Richard ni mwandishi maarufu tuu wa Uholanzi ambaye awali hakupata umaarufu wowote hadi ilipobainika kuwa alimuuwa mke wake na kuandika riwaya inayotaja undani wa uhalifu huo alioufanya mwenyewe. Alizaliwa mwaka 1937 Uholanzi, na kuuhusu kipaji chake na uwezo wake haswa wa uandishi, akiwa na umri wa miaka 18 kipaji chake kikubwa cha uandishi kilionekana. Na alikuwa anapenda sana kusoma kiasi kwamba alimaliza kusoma zaidi ya riwaya 100 za waandishi wengine akiwa na umri wa miaka 19 tuu, na alishinda tuzo nyingi za uandishi bora katika shule ya upili aliyokuwa akisoma, lakini ndoto ya Richard ilikuwa ni kuchapisha riwaya yake kwa jina lake. Richard alioa akiwa ...

ALIKATWA MKONO, LAKINI HAIKUMZUIA KUCHEZA MPIRA KWA MAFANIKIO MAKUBWA!

 Swahili Prime Ent: Mwaka 1948 Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Germany Robert Schlienz Alipata Ajali ya Gari na Kukatwa Mkono. Licha ya Ajali Hiyo Mbaya Lakini Miezi Mnne tuu Baadaye Aliendelea Kusakata Kabumbu. Alicheza Soka kwa Miaka 12 Akiwa Mlemavu. Kabla ya Hapo Alikuwa Amepigwa Risasi ya Taya Vitani na Kupona. Ilikuwa ni Augost 14, 1948 ambapo Schlienz nyota wa mpira wa miguu wa Ujerumani na nahodha wa timu ya Ujerumani ya VfB Stuttgart alikuwa akiendesha gari lake kwa kasi kwa sababu alichelewa kwenye mazoezi ya timu yake, alikuwa anaensesha huku mkono wake wa kushoto akiwa ameitoa nje ya dirisha. Wakati gari likienda kwa kasi alikutana na shimo barabarani, gari lake likapinduka na mkono wake ukasagika kabisa. Madaktari waliamua kumponya mara moja kwa kuukata mkono huo kitendo kilichomkatiaha tamaa na kuona carrier yake katika soka ilikuwa hatarini kufika mwisho. Lakini miezi minne tuu baadaye mwamba alirejea tena katika soka baada ya kupewa moyo na kocha wake Georg Wurzer huku...

MWANAMKE KATILI ALIEUWA WATU NA KUTENGENEZA SABUNI NA MIILI YA MAREHEMU

 Mwaka 1939 Leonarda alipata habari kwamba mwanawe mkubwa wa kiume na mtoto aliyempenda zaidi, Giuseppe angejiunga na Jeshi la Kifalme la Italia kilazima ili kujitayarisha kwa vita vya pili vya Dunia, hivyo aliazimia kumlinda kwa vyovyote vile mwanae huyo asijiunge na jeshi hilo. Hitimisho alilofikia lilikuwa ni kwamba usalama wake ulihitaji sadaka za kibinadamu, ushirikina. Leonarda aliwauwa wanawake watatu wa makamo Faustina Setti, Francesca Soavi na Virginia Cacioppo wote majirani zake akiamini kwamba hiyo ndio njia ya kumlinda mwanae asichukuliwe kwenda jeshini. Inaelezwa kuwa miili ya wanawake hao wote watatu alikuwa akiikatakata mmoja mmoja na kumchemsha kwenye chungu motoni huku akiweka na kemikami kadhaa ili kulainisha pishi lake hilo na baadaye kupata urojo mlaini uliofaa kutengenezea sabuni safi za cream. Baada ya kesi yake kusomwa mahakamani mwaka 1940 hatimaye alihukumiwa kifungo cha miaka 33 jela. Leonarda alifariki October 15, 1970 akiwa na miaka 76 ak...

Mwamba aliyekaa baharini zaidi ya mwaka akila samaki wabichi

 Swahili Prime Int: Anaitwa JosΓ© Salvador Alvarenga Raia wa Amerika. Mwaka 2012 Alipotelea Baharini Akiwa Katika Uvuvi. Alikaa Baharini Humo Bila Msaada Wowote Kwa Muda wa Mwaka Mmoja na Miezi Kadhaa. Katika muda huo wote Alikuwa Akishindia Samaki Wabichi Kama Chakula. Alipotea Mwaka 2012, Akaja Kukolewa Mwaka 2014. Alvarenga yeye ni mvuvi maarufu aliyejipatia umaarufu huo mwaka 2012 baada ya kupotea baharini kwa siku 438 ambazo ni sawa na mwaka mmoja na miezi miwili. Alizaliwa mwaka 1975 nchini El Salvador America ya kati. Ilikuwa ni November 17, 2012 ambapo alipanga ratiba yake ya usiku ya kwenda baharini kuvua samaki katika pwani ya kijiji cha Costa Azul kama ambavyo amekua akifanya. Hii ni katika bahari kubwa zaidi ya Pacific Mvuvi huyu mwenye uzoefu alikusudia kufanya kazi hio ya baharini kwa saa 30 ambapo alitarajia kupata papa, samaki aina ya marlin, na samaki wengine wa baharini. Mvuvi mwenzake wa siku zote hakuweza kujiunga naye, kwa hiyo akapanga badala yake amchukue Eze...

RAISI WA UGANDA IDI AMIN ALIIVYOICHOKOZA ISRAEL NA KUPIGWA VIBAYA MNO

 FM facts: Mwaka 1976 Rais wa Uganda, Dikteta Idi Amin Aliingilia Mgogoro Usiokuwa Wake (Mgogoro wa Israel na Palestina). Wiki Moja tuu Baadaye Entebbe Ikachakazwa na Kugeuka Uwanja Uliojaa Maiti na Damu Ndani ya Dakika 90 Tuu. Ni Juni 1976 ambapo ndege ya Air France Airbus A300 iliyokuwa na abiria 248 ilitekwa nyara na wanachama wawili wa kundi la Popular Front for the Liberation of Palestine - External Operations (PFLP-EO) ikiwa ni dakika chache tuu baada ya kuruka katika uwanja wa ndege wa Tel Aviv Israel ikielekea Paris. Watekaji nyara hao raia wa Palestina walikuwa wanashinikiza kuaachiliwa huru kwa wapiganaji 40 wa Kipalestina waliofungwa nchini Israel pamoja na wengine wengi waliofungwa katika nchi nyinginezo. (Hapa tayari chanzo ni mgogoro wa Palestina na Israel). Vituo vya ndege hiyo vilikuwa ni kuanzia Tel Aviv, kisha ingetua kujaza mafuta Benghazi Libya, Entebbe Uganda na baadaye moja kwa moja Paris Ufaransa, lakini sasa watekaji walikuwa tayari ndani kuidhibiti ndege h...

HAYA HAPA MATUKIO YA UTATA ZAIDI KUWAH KUTOKEA TANZANIA

 Haya ni matukio muhim yaliyotokea na kutikisa nchi 1962: Mwalimu Nyerere kujiuzuru uwaziri mkuu wakati ameijenga Tanganyika kwa heshima, wengi walishangaa kumbe alikuwa na malengo yake, 1962: kilianzishwa chuo kikuu cha kwanza UDSM pale Lumumba kabla ya kuhamia kilipo sasa hivi, 1963: Jaribio la kwanza la Kumpindua mwalimu Nyerere , kwa bahati nzuri halikufanikiwa, na Nyerere akaomba usaidizi wa waingereza, 1964 : Mapinduzi makubwa ya mfumo ndani ya jeshi , mwalimu karibia alifukuza jeshi zima na recruitment ikaanza upya chini ya jeshi la waingereza, 1964 : Kubadili jina la nchi kutoka Tanganyika na kuwa Tanzania kutokana na muungano na Zanzibar 1965 : Uanzishwaji wa Benki kuu ya Tanzania, baada ya EACB kuvunjwa, 1967: Azimio la arusha lilitikisa nchi na kuja na mpango wa utaifishaji, 1971: Tanzania iliingia mgogoro kwa mara ya kwanza na Uganda, lakin mwalimu Nyerere akajiandaa kwenda urusi kuomba silaha baada ya kugundua jamaa aliyekuja ni upuuzi, Amini mwaka huo alitikisa kiberi...

MKAKATI WA KUPITISHA DINI MOJA CHINI YA MATRIX!

  ABRAHAMIC RELIGION!  Kama unaona acha tuendelee kula bata kidogo alafu badae ndo  tutamrudia MUNGU! Uko nje ya muda! Mpaka sasa wewe umelala usingizi mzito sana na SYSTEM inakupeleka inavyotaka! Inshort unatembea mule mule kwenye MSTARI WA MATRIX!  Kipindi umeletewa intertainment kibao, mipira, betting, music na kumbi za starehe na mambo mengine ya ajabu ajabu kukukeep.busy, huko wanaendelea kupanga mipango na kuitekeleza kukuangamiza! Tayari mpaka sasa Kuna utaratibu wa kufanya Dunia nzima iwe chini ya System moja, kuanzia Kidini, kiserikali, kiuchumi na maisha yote Kwa ujumla! (NEW WORLD ODER)  Na kama mambo mengine yanavyofanyiwa kazi, Msingi wa SYSTEM YA KISHETANI ni kupitia DINI anatumia Dini kupitisha Mafundisho yake na system zake za kishetani! Na Sasa anazitumia zile dini alizozianzisha kuzileta pamoja kutengeneza DINI MOJA ITAKAYOUNGANISHA WATU KUABUDU SIKU MOJA! Mpaka sasa hilo zoezi limeanza na kimetengenezwa kitu kinaitwa ABRAHAMIC RELIGION! inaung...

🚨 BREAKING: Michael Carrick Arejea Nyumbani! Ameshinda Vita dhidi ya Solskjaer Kurithi Mikoba Man Utd! πŸ”΄πŸ‘€

SWAHILI PRIME ENT, Manchester: Ile sintofahamu ya nani atakuwa kocha wa muda wa Manchester United inakaribia kufikia kikomo. Taarifa za hivi punde zinasema kuwa klabu hiyo imekuwa na mazungumzo yenye mafanikio makubwa na kiungo wao wa zamani, Michael Carrick. Carrick anaonekana kuwa mbele ya kocha mwingine wa zamani, Ole Gunnar Solskjaer, na yuko tayari kukubali jukumu hilo la kuiongoza timu katika kipindi hiki cha mpito. Kwanini Carrick? * Anaijua vizuri falsafa ya klabu. * Alionyesha uwezo mkubwa alipokuwa kaimu kocha hapo awali kabla ya kwenda kuinoa Middlesbrough.  Mashabiki na wachezaji wana imani kubwa naye. Manchester United inatarajia kumtangaza kocha huyo mpya ndani ya saa 24 hadi 48 zijazo mara tu taratibu za mwisho zitakapokamilika. Na anatarajiwa kuiongoza timu kwenye Manchester derby, mchezo utakaochezwa Juma mosi trh 17 pale Old Trafford

KUTOKA KUZIMIA HADI USHINDI: Safari ya Eric Chelle Inayofundisha Dunia!

Katika soka, kuna wakati maumivu yanakuwa makubwa kuliko uwezo wa binadamu kustahimili. Huu ulikuwa ukweli mchungu kwa kocha Eric Chelle wakati wa mashindano ya AFCON 2023 . Wengi hawatasahau picha ya kocha huyu akimwagiwa maji kichwani baada ya kukaribia kuzimia kwa presha (stress) wakati timu yake ya Mali ikipoteza dhidi ya Ivory Coast . Dunia ilimcheka, na muda mfupi baadaye, serikali ya Mali ilimfuta kazi. Lakini kama wasemavyo, "Simba akivizia, hadhara hudhani ni mgonjwa." Leo hii, Eric Chelle amerejea kileleni akiinoa timu ya Taifa ya Nigeria , Super Eagles . Chini ya uongozi wake katika mashindano ya AFCON 2025 , Nigeria imeonekana kuwa tishio, ikicheza soka la kasi na lenye nidhamu. Safari ya Chelle inatufundisha kuwa: * Kushindwa kwa leo siyo mwisho wa maisha. * Watu wanaokucheka leo, watakupongeza kesho ukikataa kukata tamaa. * Afya ya akili na presha ni vitu halisi katika kazi yoyote ile.

MBINU ZA KIKOMANDO: JINSI MAREKANI ILIVYOMKAMATA MADURO GIZANI! πŸ•΅️‍♂️πŸ‡ΊπŸ‡Έ

Dunia bado inashangaa! Ripoti mpya zinaonyesha jinsi Marekani ilivyozima umeme nchi nzima ya Venezuela kumpata NicolΓ‘s Maduro .  Je, hii ni mwanzo wa mabadiliko makubwa Amerika Kusini au ni uonevu wa mataifa makubwa?  🚁Mambo 5 Muhimu Kuhusu Kukamatwa kwa Maduro 1. Ujasusi wa Ndani (The Mole): Marekani ilikuwa na mtu ndani kabisa ya serikali ya Maduro ambaye alitoa ramani na ratiba ya rais huyo saa 24. Huyu mtoa habari bado hajajulikana jina lake. 2. Giza Totoro (Blackout): Jeshi la Marekani (Cyber Command) liliweza kuzima umeme mji mzima wa Caracas (mji mkuu wa Venezuela) kwa kutumia mashambulizi ya kimtandao (hacking) ili kuruhusu helikopta 150 kuingia bila kuonekana. 3. Kushindwa kwa Ulinzi: Mifumo ya ulinzi wa anga ya Urusi na China iliyokuwa ikitumiwa na Venezuela ilishindwa kufanya kazi kutokana na teknolojia ya Marekani ya jamming (kuzuia mawasiliano). 4. Mapambano Mafupi: Makomando wa Marekani walimkamata Maduro akiwa anajaribu kujifungia kwenye chumba cha siri ...