ALIMCHINJA MKE WAKE NA KUANDIKA HIYO STORY KWENYE KITABU!
Swahili Prime Ent:
Richard Kleinhammer ni Mwandishi wa Vitabu wa Uholanzi, Mwaka 1991 Alimchinja Mke Wake Hannelore na Kisha Kuandika Stori Hiyo Yote ya Mauwaji Katika Kitabu Chake na Kuuza Nakala Zake. Kitabu Kinaitwa 'Jumatano Siku ya Nyama ya Kusaga', Mwaka 2000 Alikamatwa na Kutiwa Gerezani kwa Mauwaji Hayo ya Mkewe.
Richard ni mwandishi maarufu tuu wa Uholanzi ambaye awali hakupata umaarufu wowote hadi ilipobainika kuwa alimuuwa mke wake na kuandika riwaya inayotaja undani wa uhalifu huo alioufanya mwenyewe.
Alizaliwa mwaka 1937 Uholanzi, na kuuhusu kipaji chake na uwezo wake haswa wa uandishi, akiwa na umri wa miaka 18 kipaji chake kikubwa cha uandishi kilionekana.
Na alikuwa anapenda sana kusoma kiasi kwamba alimaliza kusoma zaidi ya riwaya 100 za waandishi wengine akiwa na umri wa miaka 19 tuu, na alishinda tuzo nyingi za uandishi bora katika shule ya upili aliyokuwa akisoma, lakini ndoto ya Richard ilikuwa ni kuchapisha riwaya yake kwa jina lake.
Richard alioa akiwa na umri wa miaka ishirini na tano, alimuoa msichana aitwaye Hannelore ambaye alimpenda tangu wakati wa masomo yake ya chuo kikuu.
Maisha yalikuwa yakiendelea kawaida kati ya wanandoa hao hadi mke wake Hannelore alipopotea siku moja mwaka 1991 katika mazingira ya kutatanisha.
Richard alitoa taarifa polisi kuwa mke wake ametekwa na hajui aliko, na baada ya kumtafuta kwa muda mrefu hawakuweza kumpata huku kila mtu akidhani kuwa Hannelore alikuwa ameamua kujitenga na mpenzi wake.
Mwaka 2000, miaka tisa baada ya Hannelore kutoweka, Richard aliuza nyumba yake na kuhamia nyumba nyingine ndogo na ya bei nafuu huko Amsterdam.
Siku kadhaa baadaye wanunuzi hao wa nyumba yake waliripoti kwa polisi kuwepo kwa mifupa kwenye bustani ya nyumba hiyo, na hivi siku cahche tuu baadaye Richard alikamatwa kwa uchunguzi wa tukio hilo.
Baada ya kuhojiwa sana Richard alikiri kuwa mabaki hayo ni ya mke wake Hannelore, na kwamba yeye ndiye aliyemuua ili atumie kama stori kuandika riwaya yake ambayo ni kweli ilikuwa na maelezo yote ya uhalifu huo alioufanya. Riwaya hio lilikuwa inaitwa 'Woensdag Gehaktdag', likimaanisha 'Jumatano siku ya nyama ya kusaga'.
Riwaya hiyo iliyokuwa imetoka mwaka mmoja baada ya mkewe kutoweka ilifungiwa, na mwaka 2001 Richard alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela, na alitumikia miaka miwili tu na kuachiwa kutokana na tabia nzuri gerezani.
Richard alifariki mwaka 2016 akiwa amejipumzisha katika kisiwani huko France akiwa na umri wa miaka 78.
Comments
Post a Comment