MBINU ZA KIKOMANDO: JINSI MAREKANI ILIVYOMKAMATA MADURO GIZANI! 🕵️‍♂️🇺🇸

Dunia bado inashangaa! Ripoti mpya zinaonyesha jinsi Marekani ilivyozima umeme nchi nzima ya Venezuela kumpata Nicolás Maduro

Je, hii ni mwanzo wa mabadiliko makubwa Amerika Kusini au ni uonevu wa mataifa makubwa? 


🚁Mambo 5 Muhimu Kuhusu Kukamatwa kwa Maduro


1. Ujasusi wa Ndani (The Mole): Marekani ilikuwa na mtu ndani kabisa ya serikali ya Maduro ambaye alitoa ramani na ratiba ya rais huyo saa 24. Huyu mtoa habari bado hajajulikana jina lake.


2. Giza Totoro (Blackout): Jeshi la Marekani (Cyber Command) liliweza kuzima umeme mji mzima wa Caracas (mji mkuu wa Venezuela) kwa kutumia mashambulizi ya kimtandao (hacking) ili kuruhusu helikopta 150 kuingia bila kuonekana.


3. Kushindwa kwa Ulinzi: Mifumo ya ulinzi wa anga ya Urusi na China iliyokuwa ikitumiwa na Venezuela ilishindwa kufanya kazi kutokana na teknolojia ya Marekani ya jamming (kuzuia mawasiliano).


4. Mapambano Mafupi: Makomando wa Marekani walimkamata Maduro akiwa anajaribu kujifungia kwenye chumba cha siri chenye chuma (steel safe room). Walinzi wake 32 raia wa Cuba waliuawa kwenye mapambano hayo.


5. Mpango wa Baadaye: Marekani imeonekana kupendelea kufanya kazi na Makamu wa Rais wa zamani, Delcy Rodríguez, ili kuleta utulivu badala ya kuweka wapinzani waliokuwa uhamishoni.

Comments