RAISI WA UGANDA IDI AMIN ALIIVYOICHOKOZA ISRAEL NA KUPIGWA VIBAYA MNO

 FM facts:

Mwaka 1976 Rais wa Uganda, Dikteta Idi Amin Aliingilia Mgogoro Usiokuwa Wake (Mgogoro wa Israel na Palestina). Wiki Moja tuu Baadaye Entebbe Ikachakazwa na Kugeuka Uwanja Uliojaa Maiti na Damu Ndani ya Dakika 90 Tuu.


Ni Juni 1976 ambapo ndege ya Air France Airbus A300 iliyokuwa na abiria 248 ilitekwa nyara na wanachama wawili wa kundi la Popular Front for the Liberation of Palestine - External Operations (PFLP-EO) ikiwa ni dakika chache tuu baada ya kuruka katika uwanja wa ndege wa Tel Aviv Israel ikielekea Paris.


Watekaji nyara hao raia wa Palestina walikuwa wanashinikiza kuaachiliwa huru kwa wapiganaji 40 wa Kipalestina waliofungwa nchini Israel pamoja na wengine wengi waliofungwa katika nchi nyinginezo. (Hapa tayari chanzo ni mgogoro wa Palestina na Israel).


Vituo vya ndege hiyo vilikuwa ni kuanzia Tel Aviv, kisha ingetua kujaza mafuta Benghazi Libya, Entebbe Uganda na baadaye moja kwa moja Paris Ufaransa, lakini sasa watekaji walikuwa tayari ndani kuidhibiti ndege hiyo.


Shida ilianzia pale ambapo Rais wa Uganda Idi Amini alipopewa taarifa kuhusu ujio wa ndege hio iliyotekwa katika uwanja wake wa Entebbe, ajabu akaonyesha kuwaunga mkono watekaji huku akionekana kuwakaribisha.


Baada ya kuwahamisha mateka wote kutoka kwenye ndege hadi kwenye jengo la uwanja wa ndege ambalo lilikuwa jipya, watekaji nyara waliwatenganisha Waisraeli wote na Wapalestina na kuwalazimisha kufungiwa katika vyumba tofauti.


Kwa muda wa siku mbili zilizofuata mateka 148 wakiyahudi waliachiliwa na kusafirishwa kwa ndege hadi Paris. Abiria 94 waisraeli pamoja na wafanyakazi 12 wa ndege hio (jumla 106) walibaki kama mateka katika uwanja wa ndege wa Uganda na kutishiwa kuuawa, huku bwana Idi Amini akichelekelea na kutoa sapoti.


Baada ya taarifa hizi ikabidi shirika la ujasusi la Israel Mossad liandae operation ya kuwaokoa watu wake waliotekwa Uganda, ajabu ni kwamba Jeshi la Uganda nalo likaanza kuandaa silaha ili kupambana na jeshi la Israel watakapokuja kutaka kuwaokoa watu wake.


Shirika la ujasusi la Israel (Mossad) likakiteua kikosi kazi hatari sana cha makomando nchini humo cha kuitwa Sayeret Matkal kikiwa na makomando 100 chini ya mtu hatari Yonatan Netanyahu ili kuelekea Uganda kufanikisha uokoaji.


NB: Komando Yonatan Netanyahu ni kaka wa damu kabisa wa waziri mkuu wa sasa wa Israel Benjamin Netanyahu.


Kabla ya safari ilitakiwa mpango wa uokoaji uwekwe mezani kwanza, ukasomwa uwanja mzima wa ndege wa Entebbe jinsi ulivyo nje ndani pamoja na njia zote za kuingia na kutoka. Baada ya wiki hiyo sasa safari ikaanza rasmi July 4, 1976 kuelekea Uganda huku katika ndege yao wakiwa na gari jipya sawa na lile ambalo Idi Amin hulitumia katika safari zake ndani ya nchi.


Saa kumi kamili za usiku wanajeshi katika uwanja wa ndege wa Entebbe wanashtuka kuona ndege inatua, ghafla wanaona gari ya rais inashuka kwenye ndege hiyo na kudhania kwamba pengine rais wao ndiyo yu ndani ya gari hilo bila kujua kwamba huo ni mtego wa kuwapumbaza waendelee kuzubaa.


Kabla hawajakaa sawa njugu zikaanza kumiminwa hali iliyopelekea ndani ya dakika 90 tuu za usiku huo wa saakumi zaidi ya wanajeshi 500 wa Uganda kuachwa wakiwa hawana maisha. Hata taarifa zilipofika kwa rais Amin kwamba wamevamiwa na kupelekea kuongezwa kwa wanajeshi zaidi, bado wote waliishia kuuliwa.


Katika mapambano hayo mateka 102 walifanikiwa kuokolewa, mateka wanne walifariki huku uwanja wa ndege wa Entebbe ukibaki ukiwa kama shamba lililojaa maiti na damu, hautazamiki. Lakini pia kwa bahati mbaya sana kiongozi mkuu wa makomando wa Israel Yonatan Netanyahu alipigwa risasi na kufariki uwanjani hapo, japo maiti iliuchukuliwa pia.


Baada ya makomando kumaliza kazi yao Uganda, walikwenda kutua kwa dharula nchini Kenya kujaza mafuta ndege yao hali iliyozidi kumpa hasira zaidi Amini kuona kwamba kumbe hata majirani zake Kenya wapo upande wa Israel. Akaamuru raia wa Kenya wote waliopo Uganda wauwawe!. Zaidi ya Wakenya 300 waliuwawa na wengine 3000 waliikimbia nchi hio.


Licha ya kufa kwa mahusiano ya kidiplomasia kati ya Kenya na Uganda kufuatia tukio hilo, lakini baadaye maelewano yalirejea.


Lakini pia tunaweza kusema ni kama Rais Amini aliyataka haya kwasababu katika wiki hiyo moja kabla, serikali ya Israel ilijitahidi sana kuomba watu wao waachwe huru huku ikiiomba Uganda kutoa msaada kidiplomasia, lakini Uganda ilikuwa ikikaidi.


Awali Waisraeli awali walikuwa na mpango ambapo wangewaangusha makomando wa majini kupitia Ziwa Victoria. Makomando wangepanda boti hadi uwanja wa ndege pembezoni mwa ziwa. Walipanga kuwaua watekaji nyara na baadae kuwaokoa mateka, lakini waliacha mpango huu kwa sababu waliarifiwa kwamba katoka Ziwa Viktoria kuna mamba.


Amin alikasirika mno aliposhuhudia uvamizi huo, askari 14 walikamatwa na aliwauwa kwa risasi kwa bastola yake kwa tuhuma za kushirikiana na Waisraeli huku Godwin Sule, kamanda wa kambi ya wanaanga ya Uwanja wa ndege wa Entebbe akitakiwa kunyongwa kwasabu siku ya tukio yeye alikuwa akiinjoy na mchepuko katika hoteli ya Lake Vikroria, japo alisamehewa. 


Miaka miwili baadaye, Mei 24, 1978 waziri wa kilimo wa Kenya, Bruce MacKenzie aliuawa baada ya bomu lililowekwa kwenye ndege yake kulipolipuka wakati akiondoka kwenye mkutano na Amin. Baadhi wamedai kuwa rais wa Uganda Idi Amin aliamuru maajenti wa Uganda kumuua MacKenzie ili kulipiza kisasi kwa Kenya kuhusika katika uvamizi wa Israel miaka miwili iliyopita.


Miaka ya Baadaye Mkurugenzi Mkuu wa shirika la ujasusi la Israel (Mossad) Meir Amit, aliamuru moja ya msitu uliopandwa huko Israeli uitwe kwa jina la MacKenzie. Hii ni Operation Thunderbolt.


Comments

Popular posts from this blog

Mwaka 1989 Kundi Hatari la Kihalifu la Medellin Cartel la Colombia Linalomilikiwa na Pablo Escobar Lililipua Ndege na Kuuwa Abiria Wote 107, Lengo Lao Lilikuwa ni Kumuua Mgombeaji Urais wa Nchi Hiyo Álvaro Gómez

ALIKATWA MKONO, LAKINI HAIKUMZUIA KUCHEZA MPIRA KWA MAFANIKIO MAKUBWA!

Anaitwa Chris McCandless Raia wa California US. Mwaka 1992 Akiwa na Miaka 24 Aliamua Kuingia Porini, Mbali ili Akaishi Maisha ya Asili, Maisha Kama ya Wanyama kwa Miezi 3 Kisha Arudi Nyumbani. Miezi Mitatu Baadaye Mwili Wake Ulipatikana Umeoza Porini. Inaelezwa Alikufa kwa Njaa.