MWANAMKE KATILI ALIEUWA WATU NA KUTENGENEZA SABUNI NA MIILI YA MAREHEMU

 Mwaka 1939 Leonarda alipata habari kwamba mwanawe mkubwa wa kiume na mtoto aliyempenda zaidi, Giuseppe angejiunga na Jeshi la Kifalme la Italia kilazima ili kujitayarisha kwa vita vya pili vya Dunia, hivyo aliazimia kumlinda kwa vyovyote vile mwanae huyo asijiunge na jeshi hilo.


Hitimisho alilofikia lilikuwa ni kwamba usalama wake ulihitaji sadaka za kibinadamu, ushirikina.


Leonarda aliwauwa wanawake watatu wa makamo Faustina Setti, Francesca Soavi na Virginia Cacioppo wote majirani zake akiamini kwamba hiyo ndio njia ya kumlinda mwanae asichukuliwe kwenda jeshini.


Inaelezwa kuwa miili ya wanawake hao wote watatu alikuwa akiikatakata mmoja mmoja na kumchemsha kwenye chungu motoni huku akiweka na kemikami kadhaa ili kulainisha pishi lake hilo na baadaye kupata urojo mlaini uliofaa kutengenezea sabuni safi za cream.


Baada ya kesi yake kusomwa mahakamani mwaka 1940 hatimaye alihukumiwa kifungo cha miaka 33 jela. Leonarda alifariki October 15, 1970 akiwa na miaka 76 akiwa bado anatumikia kifungo chake katika gereza hatari la wanawake la Pozzuoli huko Italia.


Vifaa kadhaa ikijumuisha chungu ambamo waathiriwa walichemshwa bado vipo mpaka sasa, vinaonyeshwa katika Jumba la makumbusho la Criminological huko Roma. Katika maelezo yake mahakamani Leonarda alisema kuwa alikuwa amepata wastani wa lita 3,000 za mchemsho wa wanawake hao alioufanya sabuni za cream.

Historia ya maisha yake inaanza huko Avellino Italia pale mamake alipobakwa na mchunga ng'ombe akiwa binti mdogo wa miaka 14. Kwa sababu hiyo familia yake ilisisitiza kuolewa na mchungaji huyu wa mifugo kwa kuogopa kashfa, na mama huyo alijifungua mtoto mwaka 1894, mtoto huyo ndiye Leonarda Cianciulli.


Baada ya baba wa mtoto Leonarda kufariki, mama yake Leonarda aliolewa tena, na Leonarda aliishi kama mtu aliyetengwa kwasababu mama yake hakumpenda baba yake kutokana na kwamba aliolewa naye baada ya kum'baka. na kutengwa huku kulimsababishia Leonarda hali ya kifafa na kudumazwa akili.


Mwaka 1917 Leonarda alipata mume bwana Raffaele Pansardi ambaye alikuwa mfanyakazi wa serikali, licha ya familia yake kukataa ndoa hii lakini yeye alisisitiza kuwa anataka kuolewa, hali hiyo ilimfanya mama yake aende siku ya harusi kumtukana binti yake na kumlaani mbele ya kila mtu, alitoa laana kuwa watoto wake wote wafe akiwa atajifungua.


Licha ya mama kuzungumza maneno makali kiasi hicho mbele za watu, lakini Leonarda hakujari, ndoa ilifungwa na mwaka 1921 walihama kabisa katika mji huo na kwenda kuishi mbali na mama yake.


Mumewe Raffaele naye alikuwa mpigaji tuu, mwaka 1927 alifungwa jela katika mji waliokuwa wanaishi wa Potenza kwa tuhuma za utapeli, na baada ya kutoka jela mwaka 1930 wakahamia huko Correggio baada ya nyumba yao kusambaratishwa na tetemeko la ardhi.


Huko Leonarda alifungua duka la sabuni na kuwa muuza sabuni maarufu sana, lakini mambo yalianza kubadilika baada ya kujiona kwamba kila ujauzito aliokua anaupata mtoto alikua anafariki wakati wa kujifungua, hali hiyo ilimtokea katika mimba tatu mfululizo.


Kwa ujumla wake Leonarda alikuwa ameshika mimba 17 wakati wa ndoa yake, lakini alipoteza watoto watatu kwa kuharibika kwa mimba. Wengine 10 walikufa katika utoto wao kwahivyo Leonarda alikuwa akiwalinda mno watoto wake wanne waliobaki. 


Hofu yake ilichochewa na onyo alilokuwa amepokea muda fulani awali kutoka kwa mtabiri, mtaalamu wa utabiri ambaye yeye alisema kwamba Leonarda angeolewa na kupata watoto ndio, lakini watoto wote wangekufa wangali wachanga.


Inaripotiwa kwamba Leonarda pia aliwahi kumtembelea mganga mmoja wa jadi na akaambiwa “Katika mkono wako wa kulia ninaona gereza, upande wako wa kushoto naona hifadhi ya wahalifu".


Kutokana na hali hiyo Leonarda akaamua nayeye kuwa mganga wa kienyeji kabisa ili kuwa karibu na tiba za kuwalinda watoto wake wa dhahabu aliokua amesalia nao, na alichanganyikiwa zaidi baada ya mwaka 1939 serikali ya Italia kutangaza kwamba wanahitaji vijana wote wa kiume waende jeshini kujiandaa na vita ya pili ya dunia.

Comments

Popular posts from this blog

Mwaka 1989 Kundi Hatari la Kihalifu la Medellin Cartel la Colombia Linalomilikiwa na Pablo Escobar Lililipua Ndege na Kuuwa Abiria Wote 107, Lengo Lao Lilikuwa ni Kumuua Mgombeaji Urais wa Nchi Hiyo Álvaro Gómez

ALIKATWA MKONO, LAKINI HAIKUMZUIA KUCHEZA MPIRA KWA MAFANIKIO MAKUBWA!

Anaitwa Chris McCandless Raia wa California US. Mwaka 1992 Akiwa na Miaka 24 Aliamua Kuingia Porini, Mbali ili Akaishi Maisha ya Asili, Maisha Kama ya Wanyama kwa Miezi 3 Kisha Arudi Nyumbani. Miezi Mitatu Baadaye Mwili Wake Ulipatikana Umeoza Porini. Inaelezwa Alikufa kwa Njaa.