MWANAMKE ALIYETABIRI MAMBO YANAYOTIMIA HADI WAKATI HUU
Swahili Prime Ent:
Moja ya Utabiri Aliouacha Baba Vanga Raia wa Bulgaria, Mmoja wa Watabiri Maarufu Kutokea Alisema Kuwa Kuanzia Mwaka 2023 Itakua ni Kawaida tuu kwa Mwanake Kwenda Maabara Kupandikizwa Mtoto na Baadaye Kuzaa. Alifariki Mwaka 1996 Akiacha Tabiri Zaidi ya 100, na Nyingizo Zinatimia.
Baba Vanga ni Nani?
Baba Vanga alikuwa mwanamke kipofu ambaye aliacha ubashiri kwa kila mwaka hadi mwaka 5079. Alizaliwa Vangelia Pandeva Dimitrova Bulgaria.
Alipokuwa na umri wa miaka 12, dhoruba ilimpiga na kumfanya apotee katika machafuko hayo na kupoteza uwezo wake wa kuona. Alipatikana siku chache baadaye akiwa kipofu.
Baba Vanga alidai kuwa alipata maono yake ya kwanza katika siku alizopotea na kimbunga hicho, na baadaye alisema uwezo wake wa kuona umebadilishwa, badala ya kuona kawada yeye anaweza kuona siku zijazo. Alifariki mwaka 1996 (85).
BAADHI YA UTABIRI WAKE ULIOTIMIA.
1️⃣Mwaka 1989 Vanga alisema: "Waamerika wataanguka baada ya kushambuliwa na ndege wa chuma, na damu isiyo na hatia itabubujika.” Wengi wameona huu ni utabiri wa mashambulizi ya kigaidi ya 9/11 huko New York mwaka wa 2001 wakati ndege mbili zilianguka kwenye jengo la Twin Towers.
2️⃣Mwaka 1980 Baba Vanga alisema kuwa jiji la Urusi la Kursk “litafunikwa na maji na ulimwengu wote utalilia,” Agosti 12, 2000 manowari ya Kursk (chombo cha kijeshi cha majini) ilizama na wanajeshi 118 walikufa.
3️⃣Mwaka 2008 Barack Obama alichaguliwa kuwa rais wa US, jambo ambalo Baba Vanga pia alitabiri. Alisema kuwa rais wa 44 wa Marekani atakuwa mweusi, Japo pia alisema angekuwa rais wa mwisho wa nchi.
4️⃣Alitabiri kuwa mwaka 2020 rais wa US atapata ugonjwa wa ajabu, wengi wanauona ni utabiri wa kweli baada ya rais Trump kuambukizwa Covid-19 mwaka huo, japo alitabiri zaidi kuwa angepata ukiziwi kutokana na ugonjwa huo.
BAADHI YA UTABIRI WA MIAKA YA MBELENI.
1️⃣Dunia itakumbwa na njaa kali kati ya mwaka 2025 hadi 2028.
2️⃣Mwaka 2046 binadamu atakuwa anaweza kutengenezwa (Cloning) viwandani.
3️⃣Mwaka 2066 Roma itakuwa chini ya dola ya kiislamu baada ya kuanza kuishika dunia kiuchumi tangu mwaka 2043.
4️⃣Mwaka 2164 wanyama wengi watakuwa na mwonekano wa nusu binadamu.
5️⃣Mwaka 2167 kutazuka dini mpya, na itavuna watu wengi.
6️⃣Mwaka 2371 kutakua na njaa kali duniani.
7️⃣Mwaka 3005 kutakua na vita kubwa katika sayari ya Mars, baada ya watu wengi kuhamia huko.
8️⃣Mwaka 5079 ndiyo utakua mwisho wa Dunia.
Hata hivyo kuna utabiri wake kadhaa haujatimia ukiwemo wa kutokea kwa vita ya tatu ya dunia 2010-2014.
Comments
Post a Comment