MWAMBA ALIKUWA HAFANYI MAZOEZI LAKINI ANATUPIA KILA MECHI

Unasema Wachezaji Wengi wa Soka wa Sasa ni Watukutu? Karibu Nikusimulie Kisa cha Mchezaji Giuseppe Meazza Raia wa Italia. Yeye Alikuwa Hafanyi Mazoezi na Timu Yake Lakini Anatupia Kila Mechi, Anavuta Sigara Hata Kwenye Half Time ya Mechi na Hakuna Anaesema Lolote, San Siro Kuna Jina Lake.


Meazza alizaliwa mwaka 1910 huko Italia, alipokuwa mchezaji wa soka alizoea kuvuta sana sigara kiasi kwamba alikuwa anaweza kuvuta sigara wakati wa mapumziko ya mechi mbele ya wachezaji wenzake na kocha wake. Wachezaji walimzoea mchezaji huyo na staili yake.


Meazza alikuwa akifanya mazoezi na timu yake ya Inter Milan kwa siku moja tu kwa wiki au asifanye kabisa, lakini kwenye mechi anakupa kila kitu unachotaka uwanjani, wachezaji na mashabiki wa klabu yake ya Inter Milani walimpachika jina la 'The Miracle'.


Moja ya matukio ya ajabu ambayo nimesoma kuhusu mchezaji huyo ni katika mechi ya dabi kati ya timu yake ya Inter Milan na AC Milan.


Picha linaanza jamaa anammka nyumbani dakika 5 tuu kabla ya mechi kuanza, akavaa nguo zake safi na kwenda uwanjani, wakati akielekea uwanjani alikutana na rafiki yake na akakaa naye kwenye cafe karibu na uwanja wakati wa mechi wakipata kahawa, huku ndani mechi inaendelea. 


Dakika 45 zilipomalizika jamaa akaingia dressing room kuungana na timu, kipindi cha pili kinaanza kocha wake akamuingiza dakika ya 72 na hapo alifunga hat-trick ndani ya dakika 10 na kisha akaomba kutolewa.


Kocha akamfanyia sub dakika ya 86 na moja kwa moja jamaa akarudi nyumbani kuendelea kulala.


Meazza alikua mchezaji matata sana, yeye ndiye alichangia kwa kiasi kikubwa Italia kushinda Kombe la Dunia mara mbili mfululizo mwaka 1934 na 1938 huku akishinda tuzo za mchezaji bora mara kadhaa. 


Meazza alifariki mwaka 1979 akiwa na umri wa miaka 69. Wakati yupo Inter Milan alifunga goli 284 katika michezo 408, lakini pia alivitumikia vilabu vya Juventus, AC Millan na Atalanta kati ya mwaka 1927-1947. 


Katika ligi tano kubwa Ulaya, hawa ndio wachezaji wenye hattricks nyingi zaidi katika historia ya football huku jamaa naye akiwemo!:


1. Lionel Messi (36) La Liga

2. Cristiano Ronaldo (34) La Liga

3. Thadée Cisowski (22) Ligue 1

4. Giuseppe Meazza (17) Seria A *

5. Mario Gomez (12) Bundersliga


March 3, 1980 uwanja wa nyumbani wa timu za Inter Milan na AC Milan wa San Siro unaoingiza mashabiki 80,000 ulipewa rasmi jina la Stadio Giuseppe Meazza kumuenzi mwamba. San Siro ni jina la zamani. Italia wanamtambua Meazza kama G.O.T wao.


Swahili Prime Ent

Comments

Popular posts from this blog

Mwaka 1989 Kundi Hatari la Kihalifu la Medellin Cartel la Colombia Linalomilikiwa na Pablo Escobar Lililipua Ndege na Kuuwa Abiria Wote 107, Lengo Lao Lilikuwa ni Kumuua Mgombeaji Urais wa Nchi Hiyo Álvaro Gómez

ALIKATWA MKONO, LAKINI HAIKUMZUIA KUCHEZA MPIRA KWA MAFANIKIO MAKUBWA!

Anaitwa Chris McCandless Raia wa California US. Mwaka 1992 Akiwa na Miaka 24 Aliamua Kuingia Porini, Mbali ili Akaishi Maisha ya Asili, Maisha Kama ya Wanyama kwa Miezi 3 Kisha Arudi Nyumbani. Miezi Mitatu Baadaye Mwili Wake Ulipatikana Umeoza Porini. Inaelezwa Alikufa kwa Njaa.