ALIKATWA MKONO, LAKINI HAIKUMZUIA KUCHEZA MPIRA KWA MAFANIKIO MAKUBWA!

 Swahili Prime Ent:

Mwaka 1948 Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Germany Robert Schlienz Alipata Ajali ya Gari na Kukatwa Mkono. Licha ya Ajali Hiyo Mbaya Lakini Miezi Mnne tuu Baadaye Aliendelea Kusakata Kabumbu. Alicheza Soka kwa Miaka 12 Akiwa Mlemavu. Kabla ya Hapo Alikuwa Amepigwa Risasi ya Taya Vitani na Kupona.


Ilikuwa ni Augost 14, 1948 ambapo Schlienz nyota wa mpira wa miguu wa Ujerumani na nahodha wa timu ya Ujerumani ya VfB Stuttgart alikuwa akiendesha gari lake kwa kasi kwa sababu alichelewa kwenye mazoezi ya timu yake, alikuwa anaensesha huku mkono wake wa kushoto akiwa ameitoa nje ya dirisha.


Wakati gari likienda kwa kasi alikutana na shimo barabarani, gari lake likapinduka na mkono wake ukasagika kabisa. Madaktari waliamua kumponya mara moja kwa kuukata mkono huo kitendo kilichomkatiaha tamaa na kuona carrier yake katika soka ilikuwa hatarini kufika mwisho.


Lakini miezi minne tuu baadaye mwamba alirejea tena katika soka baada ya kupewa moyo na kocha wake Georg Wurzer huku akiwa na mkono mmoja, mechi yake ya kwanza ilikuwa ni dhidi ya viongozi wa ligi na mabingwa watetezi Bayern Munich December 5, 1948 ambapo Schlienz aliiongoza timu yake kushinda 2-1.


Schlienz alicheza mechi 391 za ligi akiwa na Stuttgart akifunga mabao 143. Alishinda mataji mawili ya Bundesliga mwaka 1950 na 1952 pamoja na Vikombe viwili vya Ujerumani mwaka 1954 na1958 akiwa na VfB Stuttgart. Alicheza mechi 3 na timu ya taifa ya Ujerumani katika nyakati tofauti.


Kumbuka kwamba kabla ya hayo yote Schlienz alipigwa risasi ya taya wakati akishiriki katika vita ya pili ya dunia kati ya nchi yake ya Germany dhidi ya Urusi. Baada ya Schlienz kuumia vitani alirudishwa nyumbani ambako alipata matibabu na kupona, kabla ya kwenda vitani alikuwa anaichezea timi ya mtaani kwao ya FV Zuffenhausen.


Mwaka 1944 baada Schlienz kuona wachezaji wengi wa timu yake ya zamani wamefatiki vitani, akaanza kufanya mazoezi ya mpira wa miguu na klabu ya soka ya Stuttgart kabla ya viongozi wa timu hiyo kumkubali na baadaye kusajiriwa rasmi na timu hiyo.


Schlienz Alifariki June 18, 1995 huko Dettenhausen, Germany akiwa na umri wa miaka 71, alikuwa amecheza soka kwa miaka 20, miaka 12 akicheza bila mkono mmoja.

Comments

Popular posts from this blog

Mwaka 1989 Kundi Hatari la Kihalifu la Medellin Cartel la Colombia Linalomilikiwa na Pablo Escobar Lililipua Ndege na Kuuwa Abiria Wote 107, Lengo Lao Lilikuwa ni Kumuua Mgombeaji Urais wa Nchi Hiyo Álvaro Gómez

Anaitwa Chris McCandless Raia wa California US. Mwaka 1992 Akiwa na Miaka 24 Aliamua Kuingia Porini, Mbali ili Akaishi Maisha ya Asili, Maisha Kama ya Wanyama kwa Miezi 3 Kisha Arudi Nyumbani. Miezi Mitatu Baadaye Mwili Wake Ulipatikana Umeoza Porini. Inaelezwa Alikufa kwa Njaa.