SIMBA WALIOKWAMISHA UJENZI WA RELI KWA MWAKA MZIMA
Swahili Prime Ent
Kwa Mujibu wa Taarifa ya Uchunguzi, Mwaka 1898 Simba Wawili Wakali Walidaiwa Kutumwa Kwa Makusudi ili Wakawauwe Wafanyakazi Waliokuwa Wanajenga Reli ya Kenya - Uganda na Kukwamisha Ujenzi Huo kwa Karibia Mwaka Mzima. Simba Hao Wanadaiwa Kuwala Wafanyakazi 140.
Katikati ya machi 1898 usiku, wafanyakazi katika mradi wa reli ya Uganda, ambayo inaunganisha na Kenya, walishambuliwa na simba wawili na kuibuka mauaji ya kutisha zaidi ya mnyama kuwashambulia binadamu katika historia.
Iweje itajwe kuwa simba walitumwa? Madhara na mwisho wake ulikuwaje?
Inaelezwa kuwa Machi 1898 simba wawili waliwavamia wafanyikazi usiku wa manane katika kambi yao na kusababisha vifo vya wafanyikazi 140 wa Kiafrika na Wahindi, na iliainishwa kama mauaji mabaya zaidi kufanywa na mnyama dhidi ya wanadamu katika historia.
Lakini nyuma ya pazia inaelezwa kuwa sababu ya mauaji hayo ni simba hao kutumwa, kusogezwa makusudi karibu na mradi ili wawashambulie wafanyakazi kwasababu wahusika wa mradi huo (waingereza) waliamua kutoa vibarua wengi nchini India na sio wazawa wa Kenya, hivyo ilikuwa ni kama kulipa kisasi.
Inaelezwa kuwa mkoloni uingereza aliamua kuleta karibia wafanyakazi 36,000 kutoka India na kuwaacha wakenya na waafrika bila kazi jambo lililowaudhi wenyeji na kuamua kuwasogezea wanyama hao wakali wawamalize kwa makusudi.
Mradi huu uliopangwa kukamilisha reli kutoka mombasa kupitia hifadhi ya taifa ya Tsavo Kenya mpaka Uganda ulianza mwaka 1895, lakini kutokana na maafa hayo makubwa ulilazimika kusimamishwa kwa miezi 9 ya machi 1898 mpaka December 1898 ulipoendelea tena.
Utulivu ulikuja baada ya Kanali John Patterson wa Uingereza kufika nchini humo na kufanikiwa kuwaua simba hao wawili na ngozi zao kugeuzwa kuwa zulia ambalo aliliuza kwa Field Museum huko Chicago US kwa pauni 5,000 sawa na laki saba za Kenya au Milioni 14 za TZ.
Mwaka 1952 ilitoka filamu ya Bwana Devil, na mwaka 1996 ilitoka filamu ya The Ghost and The Darkness, filamu hizi zote kutoka Amerika zimeelezea simulizi ya kweli kabisa juu ya simba hawa waliosumbua kwa karibia mwaka mzima katika misitu ya Tsavo Kenya mwaka 1898.
Kanali John mwenyewe pia mwaka 1907 aliandika kitabu kuhusu simba hawa alichokiita The Man-eaters of Tsavo.
Reli hiyo yenye urefu wa kilomita 1056 ilitumia miaka 34 kukamilika, licha ya awali kumilikiwa na serikali ya uingereza lakini kwasasa inamilikiwa na mamlaka za reli za Kenya na Uganda.
Comments
Post a Comment