Mwamba aliyekaa baharini zaidi ya mwaka akila samaki wabichi

 Swahili Prime Int:

Anaitwa José Salvador Alvarenga Raia wa Amerika. Mwaka 2012 Alipotelea Baharini Akiwa Katika Uvuvi. Alikaa Baharini Humo Bila Msaada Wowote Kwa Muda wa Mwaka Mmoja na Miezi Kadhaa. Katika muda huo wote Alikuwa Akishindia Samaki Wabichi Kama Chakula. Alipotea Mwaka 2012, Akaja Kukolewa Mwaka 2014.


Alvarenga yeye ni mvuvi maarufu aliyejipatia umaarufu huo mwaka 2012 baada ya kupotea baharini kwa siku 438 ambazo ni sawa na mwaka mmoja na miezi miwili. Alizaliwa mwaka 1975 nchini El Salvador America ya kati.


Ilikuwa ni November 17, 2012 ambapo alipanga ratiba yake ya usiku ya kwenda baharini kuvua samaki katika pwani ya kijiji cha Costa Azul kama ambavyo amekua akifanya. Hii ni katika bahari kubwa zaidi ya Pacific


Mvuvi huyu mwenye uzoefu alikusudia kufanya kazi hio ya baharini kwa saa 30 ambapo alitarajia kupata papa, samaki aina ya marlin, na samaki wengine wa baharini. Mvuvi mwenzake wa siku zote hakuweza kujiunga naye, kwa hiyo akapanga badala yake amchukue Ezequiel Córdoba kijana wa umri wa miaka 23 asiye na uzoefu. 


Muda mfupi baada ya kupanda mashua yao ya injini moja iliyokuwa na jokovu kubwa la kuhifadhia samaki, ilianza kupeperushwa na dhoruba kubwa iliyochukua siku tano mfululizo na kupelekea injini na vifaa vingi kuharibiwa.


Ingawa walikuwa wamevua karibu kilo 500 za samaki wabichi, lakini walilazimika kuwatupa wote baharini ili kufanya mashua kuwa nyepesi. Alvarenga alifaulu kumpigia simu bosi wake kuomba usaidizi kabla ya betri ya redio hiyo kuzima, lakini msaada haukupatikana.


Na kwa kuwa mashua haikuwa na matanga wala makasia, haikuwa na nanga, haikuwa na taa za kuelea, ilianza kupeperuka kiurahisi na upepo kuelekea ndani zaidi ya bahari.


Sehemu kubwa ya zana za uvuvi pia zilipotea au kuharibiwa na dhoruba na kuwaacha wakiwa na vifaa vichache tu vya msingi pamoja na chakula kidogo.


Kwa mujibu wa Alvarenga mwenyewe, alisema mwenzake Córdoba ilipoteza maisha miezi minne tuu katika safari hio wakiwa ndani ya bahari baada ya kuugua kutokana na chakula kibichi walichokua wanakula na hatimaye kufa kutokana na njaa kwa kukataa kula.  


Alvarenga alisema kwamba alifikiria kujiua kwa siku nne mfululizo baada ya rafiki yake huyo Córdoba kufa, lakini imani yake  ilimzuia kufanya hivyo na akaendelea kupambania uhai wake huku matumaini ya kuokolewa yakiendelea kuishi.


Alisimulia kwamba Córdoba alimfanya aahidi kutokula maiti yake baada ya kufa, kwa hiyo akaiweka kwenye mashua. Anasema Katika nyakati fulani alikuwa anazungumza na maiti, na baada ya siku sita aliogopa kwamba atakuwa kichaa, hivyo akaitupa maiti hiyo baharini.


Hadi miezi hio minne inaisha mwamba alikuwa anaishi kwa shibe ya samaki wabichi, kasa, ndege wadogo, papa na maji ya mvua. 


Alvarenga alisema kwamba aliziona meli nyingi za kontena zinazopita bahari lakini hakuweza kuomba msaada kutokana na kuwa mbali. Baada ya kutaabika kwa miezi 14 hatimaye aliiona ardhi, kilikuwa ni kisiwa kidogo cha Ebon Atoll kilichopo zaidi ya kilomita 10,000 kutoka pwani, na hio ilikuwa ni zaidi ya siku 400 zimepita, Januari 30, 2014.


Aliacha mashua yake na kuogelea hadi ufukweni kwa furaha akiwa mtupu ambako aliingia kwenye nyumba inayomilikiwa na wenandoa na kupatiwa msaada . Safari ya Alvarenga ilikuwa imechukua siku 438 akiwa katikati ya bahari huku akila samaki wabichi.


Wazazi wa Alvarenga ambao hawakuwa wamewasiliana naye kwa muda mrefu, walikuwa na hofu kwamba alikuwa amekufa muda mrefu baada ya kutoweka, huku wazazi wa Córdoba wakimtuhumu vikali Alvarenga kwamba alikuwa amemuuwa kijana wao na kumfanya nyama kutokana na kukosa chakula.


Wazazi hao walifika mbali zaidi na kumfungulia mashtaka mahakamani Alvarenga wakidai fidia ya pesa walizozitaja kuwa ni $1,000,000 kwa kuamini huko kuwa kijana wao alikuwa amefanywa mishkaki na Alvarenga wakati huo wakiwa matatizoni. Licha ya tuhuma hizo lakini mwamba alikataa kulipa.


Comments

Popular posts from this blog

Mwaka 1989 Kundi Hatari la Kihalifu la Medellin Cartel la Colombia Linalomilikiwa na Pablo Escobar Lililipua Ndege na Kuuwa Abiria Wote 107, Lengo Lao Lilikuwa ni Kumuua Mgombeaji Urais wa Nchi Hiyo Álvaro Gómez

ALIKATWA MKONO, LAKINI HAIKUMZUIA KUCHEZA MPIRA KWA MAFANIKIO MAKUBWA!

Anaitwa Chris McCandless Raia wa California US. Mwaka 1992 Akiwa na Miaka 24 Aliamua Kuingia Porini, Mbali ili Akaishi Maisha ya Asili, Maisha Kama ya Wanyama kwa Miezi 3 Kisha Arudi Nyumbani. Miezi Mitatu Baadaye Mwili Wake Ulipatikana Umeoza Porini. Inaelezwa Alikufa kwa Njaa.