ALIANZA UJAMBAZI AKIWA NA MIAKA KUMI, JAMBAZI SUGU KUTOKA INDIA

 Swahili Prime Ent

Anaitwa Koose Munisamy Veerappan raia wa India aliyezaliwa 18 January 1952. Unaambiwa India waliwahi kutokea majambazi sugu na kudhibitiwa, lakini huyu ndio alikuwa kiboko. Alifanya shughuli za uhalifu kwa miaka 42 kabla ya kudhibitiwa na kuuwawa Oktoba 18, 2004 akiwa na miaka 52.


Veerappan ni nani? Kila kitu kumhusu yeye kipo hapa


Veerappan aliyezaliwa huko Coimbatore, India alianza kazi yake ya uhalifu tangu akiwa na umri wa miaka 10 kwa msaada wa mjomba wake Saalvai Gounder, walikuwa wanauwa tembo na kuvuna pembe za ndovu na kuuza kimagendo huku makazi yao makubwa yakiwa misituni, na baada ya muda alitengana na mjomba wake na kuanza kujitegemea.


Rekodi inaonyesha kuwa katika wakati wake wote kama muhalifu 1962–2004 ameuwa zaidi ta Tembo 900, lakini ukweli ni kwamba ameuwa kati ya tembo 2000 - 3000, ameuwa watu 184 wakiwepo askari 97 na maafisa wa misituni huku akiigharimu serikali ya India zaidi ya $ 330 milioni kufanikisha kumtia nguvuni (zaidi ya TZS Bilion 750).


Unaambiwa kuwa licha ya kufaidika sana na uvunaji haramu wa pembe za ndovu, lakini pia alikuwa akiwateka wanasiasa wanaoonyesha kumsemea kwa ubaya huku akichukua pesa na mali zao na kuzigawa kwa wananchi. Hii ilipelekea Veerappan kupata sapoti kutoka hata katika vyama vya kisiasa kikiwemo chama cha Paattali Makkal Katchi na mashirika binafsi.


Mauwaji yake ya kwanza kabisa aliyafanya akiwa na umri wa miaka 17, na aliendelea kumuuwa kila aliyeonekana kuvalia njuga akamaatwe, mwaka 1972 akiwa na miaka 20 alikamatwa na jeshi la polisi na kufungwa maisha, lakini miaka 15 baadaye (1987) alitoroka na kua kama kidonda kilichotiwa ndimu.


Mmoja wa watu wa serikali aliowauwa alikuwa ni bosi wa idara ya misitu wa India Pandillapalli Srinivas aliyemuuwa November 1991.


Veerappan aliyeendelea kumuuwa kila mtu aliyeonekana ni mtoa taarifa wa Polisi juu yake, aliendelea kuuwa askari na maafisa misitu kila walipojaribu kumfuatilia mpaka serikali ya India ikaamua kupiga marufuku kwa muda vikosi vyake vya usalama kuendelea kumfuatilia.


July 30, 2000 Veerapan alimteka nyara mkali wa filamu nchini humo Rajkumar kama onyo kwa serikali waache kumfuatilia, na baada ya serikali kuacha akamuachilia Rajkumar November 15, 2000 ikiwa ni siku 108 baada ya kumteka.


Mkali huyo wa filamu za Appu na Aakasmka alifariki mwaka 2006 (76) akiwa amekaa kwenye kochi nyumbani kwake, baada ya kifo macho yake yalitolewa na kupandikizwa kwa watu wawili wenye matatizo ya kuona.


Katika mkutano wa kwanza na waandishi wa habari baada ya kuachiliwa kwake, marehemu Rajkumar alisema kwamba kipindi kizima akiwa mateka ni 'Script kamili ya filamu ya kutisha, na alizungumza hayo kwa mara ya kwanza mwaka 2004 baada ya Veerappan kuuwawa.


Inaelezwa kuwa tukio la Rajkumar kutekwa na Veerappan kwa miezi hiyo mitatu linabaki kuwa moja ya matukio mabaya yaliyoishtua nchi ya India katika historia ya nchi hiyo.


Agosti 25, 2002 Veerappan alimteka nyara H. Nagappa, waziri wa zamani wa India, Nagappa alikuwa waziri wa masoko ya kilimo kati ya 1996 - 1999. Vikosi maalum vya majeshi vya miji ya Karnataka na Tamil Nadu vilifanya kazi na polisi kusaidia kumuokoa waziri Nagappa, lakini hawakuweza.


Hatimae waziri Nagappa alipatikana akiwa ameuwawa miezi mitatu baadaye katika msitu wa Karnataka, Veerappan ndiye aliyemuuwa waziri huyo ikiwa ni mwendelezo wa maonyo ya kutofuatiliwa.


Oktoba 18, 2004 Veerappan na washirika wake watatu waliuawa na kikosi maalum cha jeshi, karibu na kijiji cha Papparapatti, Tamil Nadu. 


Baada ya mapigano ya muda mrefu Veerappan na watu wake walijeruhiwa na kuingizwa kwenye gari la wagonjwa na polisi kwa kisingizio cha kuwapeleka hospitalini kwa matibabu, lakini kikosi hicho kiliishambulia gari hio ya wagonjwa kwa makusudi ili kupoteza kabisa maisha ya jambazi huyo sugu pamoja na wenzake.

Comments

Popular posts from this blog

Mwaka 1989 Kundi Hatari la Kihalifu la Medellin Cartel la Colombia Linalomilikiwa na Pablo Escobar Lililipua Ndege na Kuuwa Abiria Wote 107, Lengo Lao Lilikuwa ni Kumuua Mgombeaji Urais wa Nchi Hiyo Álvaro Gómez

ALIKATWA MKONO, LAKINI HAIKUMZUIA KUCHEZA MPIRA KWA MAFANIKIO MAKUBWA!

Anaitwa Chris McCandless Raia wa California US. Mwaka 1992 Akiwa na Miaka 24 Aliamua Kuingia Porini, Mbali ili Akaishi Maisha ya Asili, Maisha Kama ya Wanyama kwa Miezi 3 Kisha Arudi Nyumbani. Miezi Mitatu Baadaye Mwili Wake Ulipatikana Umeoza Porini. Inaelezwa Alikufa kwa Njaa.