JIWE LILILOTABIRIWA KUIPIGA DUNIA NA KUUA KILA KIUMBE!

 Swahili Prime Ent:

Mwaka 1907 Dunia Iliingia Kwenye Hofu Kubwa Baada ya Kutangazwa Kuwa Mwaka 1910 Jiwe Kubwa Lenye Gesi Kali Litaonekana Angani, Litapasuka na Gesi Yake Itauwa Kila Kiumbe Kilichopo Duniani. Ni Kweli Mwaka 1910 Jiwe Hilo Lilionekana na Watu Wengi Kufa kwa Mshtuko Akiwemo Mfalme wa Uingereza. 

Kutokana na kuanza kukua kwa teknolojia, wataalamu wengi wa dunia walianza kutumia vyombo vya kitaalamu kugundua nini kinaweza kutokea mbeleni. katika upande wa hali ya hewa na kwingineko, na hapo ndipo mwanaanga maarufu wa Ufaransa Camille Flammarion alipotangaza hatari kubwa inayotarajia kuikumbwa dunia mwaka huo 1910.


Mwaka 1907 Flammarion alitangaza kuwa kuna jiwe kubwa mfano wa nyota lenye gesi yenye sumu hatari ya cyanogen litapasuka angani mwaka 1910 na gesi yote itasambaa duniani na kuondoa maisha ya kila kiumbe kilichopo ndani ya dunia.


Watu waliuamini mwisho huo wa dunia kwani ni kweli jiwe hilo kubwa linaloitwa Halley's Comet kitaalamu lilikuwa likitokea tangu kale kila baada ya miaka 75 au 76, hivyo kwa mwaka huo wa 1910 ilikuwa ndio mwaka wa 76 tangu litokee kwa mara ya mwisho na ilikuwa ni lazima litokee tena kama ambavyo limekua likitokea kila baada ya miaka hiyo, lakini ikaaminiwa kuwa jiwe la awamu hii litaipasukia dunia.


Habari zikasambaa duniani kote kuwa tarehe yoyote ndani ya mwaka 1910 dunia itafika mwisho kwa kila kiumbe kusambaratishwa na gesi hio yenye sumu kali, dunia ilitandwa na hofu kubwa mno kwa miaka hio mitatu, na kama kuna kipindi Mungu alikumbukwa sana katika dunia hii basi ni katika kipindi hicho.


Hatimaye Mei 6, 1910 Helley's Comet ikaonekana angani duniani kote, ilikuwa ni mfano wa jiwe kubwa sana lenye mkia, na ukijumlisha na taarifa za toka awali kwamba jiwe hilo litapasuka na gesi yake kuuwa viumbe vyote duniani basi lilipoonekana tuu watu wengi walianza kufa kwa mshtuko hata kabla halijapasuka akiwemo mfalme wa Uingereza Edward VII.


Jiwe hilo kubwa liliendelea kuelea angani karibu kabisa na uso wa dunia mpaka Mei 18, 1910 likiwaacha watu wengi wakihesabia siku zao za kuishi, huku wengine wakichimba mahandaki marefu ya kujificha ili gesi hio mbaya isiwafikie.


Lakini kwa bahati hatimaye jiwe hilo lilipotelea angani kupitia Ufaransa bila kuleta madhara yeyote kwa mtu yeyote.


Halley's Comet hutokea kila baada ya miaka 75 au 76, kwa mara ya mwisho ilitokea mwaka 1986 na linatarajiwa kutokea tena mwaka 2061.


Linaitwa Halley ili kumuenzi mwanaanga wa Uingerea Edmond Halley ambaye yeye ndio alikuwa mtaalamu wa kwanza kutabiri kuwa jiwe hilo litakua likitokea angani kila baada ya miaka 75 au 76, aliligundua hilo mwanzoni mwa miaka ya 1700

Comments