SIRO NZITO:JINSI FAMILIA YA GLAZER ILIVYOICHUKUA MANCHESTER UNITED KIMAFIA NA KUIINGIZA KWENYE MADENI MAKUBWA!
Swahili Prime Ent
Leo tunaitazama historia ya kushtua ya jinsi bilionea Malcolm Glazer alivyofanikisha ununuzi wa Manchester United kati ya mwaka 2003 na 2005. Huu ulikuwa ununuzi uliogubikwa na malalamiko mengi ambayo hadi leo yamesababisha vuguvugu la Glazers Out.
Hatua kwa Hatua ya Ununuzi:
1. Mwanzo Mdogo (Machi 2003): Malcolm Glazer alianza kwa kununua hisa ndogo tu ya 2.9% kwa takriban pauni milioni 9 (£9M). Wakati huo, United ilikuwa kampuni iliyoorodheshwa kwenye soko la hisa.
2. Ujanja wa Soko la Hisa:Kwa kipindi cha miaka miwili, Glazer aliendelea kununua hisa kidogo kidogo sokoni hadi akafikia kiwango cha kuanza kuidhibiti klabu.
3. Mapinduzi ya Mwaka 2005: Mwezi Mei 2005, familia ya Glazer ilikamilisha ununuzi wa karibu 98% ya klabu kwa thamani ya pauni milioni 790 (£790M).
Kwanini Mashabiki Walikasirika? (Leveraged Buyout):
Hapa ndipo penye siri ya madeni ya United. Glazer hakutumia pesa yake yote mfukoni. Badala yake:
Alikopa kiasi kikubwa cha fedha (takriban pauni milioni 270) ili kununua klabu.
Ajabu ya Mwaka: Deni hilo alilolitumia kununua klabu, alilihamishia kwa klabu yenyewe! Manchester United, ambayo hapo awali haikuwa na deni hata shilingi moja, ghafla ikawa inadaiwa mamia ya mamilioni.
Hii ilisababisha klabu kuanza kulipa riba ya zaidi ya pauni milioni 60 kila mwaka, pesa ambayo ingeweza kutumika kununua wachezaji au kuboresha uwanja.
Mfumo huu wa Leveraged Buyout ndio unawafanya mashabiki wahisi klabu inatumiwa kama shamba la bibi na wamiliki hao huku ikizidiwa na madeni.
VITA YA MADARAKA: Sir Jim Ratcliffe vs Familia ya Glazer – Nani Haswa Ndiye Bosi wa Manchester United Kwa Sasa?
Baada ya kuelewa jinsi Glazers walivyoingia kimafia mwaka 2005, swali kubwa ambalo kila shabiki wa United anajiuliza ni: Je, Sir Jim Ratcliffe amekuja kuiokoa Man utd au ni mshirika wa Glazers?
Huu hapa ni mchanganuo wa nani anashikilia mpini na nani anashikilia makali kwa sasa:
1. Nguvu ya Sir Jim Ratcliffe (Mwenye Maamuzi ya Soka):
Ingawa SJR anamiliki takriban 27.7% tu ya hisa za klabu, mkataba wake na Glazers unampa mamlaka kamili juu ya Shughuli zote za Soka (Football Operations).
* Hii ina maana yeye ndiye anayeamua nani asajiliwe, nani awe kocha, na jinsi ya kuboresha uwanja wa Old Trafford.
* Glazers kwa sasa wamekaa pembeni kwenye masuala ya uwanjani.
2. Nguvu ya Familia ya Glazer (Wamiliki wa Hisa na Faida):
Glazers bado wanamiliki hisa nyingi zaidi (zaidi ya 60%). Hii inamaanisha:
* Bado wanapata sehemu ya faida (dividends) klabu ikitengeneza pesa.
* Wana nguvu kwenye masuala ya kibiashara na udhamini (Commercial & Sponsorships).
* Kisheria, bado wao ndio Wamiliki Wakuu, lakini wamekubali kutoingilia maamuzi ya soka ili kupunguza hasira za mashabiki.
3. Je, Deni la Glazer Limeisha?
Hapa ndipo penye changamoto. Sir Jim ameweka takriban $300 million kwa ajili ya ukarabati, lakini yale madeni ya zamani ya Glazer bado yapo kwenye vitabu vya klabu. SJR anajaribu kusafisha uongozi (kwa kuleta watu kama Omar Berrada na Jason Wilcox) ili klabu ijiendeshe kitalamu zaidi na kuanza kulipa madeni hayo kwa kasi.
Kwa sasa, Manchester United ina marais wawili: Mmoja wa Pesa (Glazer) na Mmoja wa Soka (Ratcliffe). Mashabiki wana matumaini kuwa Ratcliffe atafanikiwa kuiondoa klabu mikononi mwa Glazers jumla hapo mbeleni.
Comments
Post a Comment