🚨 BREAKING: Michael Carrick Arejea Nyumbani! Ameshinda Vita dhidi ya Solskjaer Kurithi Mikoba Man Utd! 🔴👀
SWAHILI PRIME ENT, Manchester: Ile sintofahamu ya nani atakuwa kocha wa muda wa Manchester United inakaribia kufikia kikomo. Taarifa za hivi punde zinasema kuwa klabu hiyo imekuwa na mazungumzo yenye mafanikio makubwa na kiungo wao wa zamani, Michael Carrick.
Carrick anaonekana kuwa mbele ya kocha mwingine wa zamani, Ole Gunnar Solskjaer, na yuko tayari kukubali jukumu hilo la kuiongoza timu katika kipindi hiki cha mpito.
Kwanini Carrick?
* Anaijua vizuri falsafa ya klabu.
* Alionyesha uwezo mkubwa alipokuwa kaimu kocha hapo awali kabla ya kwenda kuinoa Middlesbrough.
Mashabiki na wachezaji wana imani kubwa naye.
Manchester United inatarajia kumtangaza kocha huyo mpya ndani ya saa 24 hadi 48 zijazo mara tu taratibu za mwisho zitakapokamilika.
Na anatarajiwa kuiongoza timu kwenye Manchester derby, mchezo utakaochezwa Juma mosi trh 17 pale Old Trafford
Comments
Post a Comment