MFUNGWA HATARI ALIYETOROKA GEREZANI KWA KUTUMIA UZI!

 Swahili Prime Ent:

Mfungwa Robert Dale Shepard Raia wa US Aliyetumia Kamba za Kusafishia Meno Kutoroka Katika Gereza la South Central Regional Jail Virginia kwa Kukwea Ukuta wa Futi 18 Mwaka 1994. Alifuma Kamba ya Futi 20.

June 29, 1994 mfungwa Robert Dale Shepard (34) aliyekuwa anatumikia kifungo katika gereza moja mashariki mwa Virginia US, alifanikiwa kutoroka gerezani kwa kupanda ukuta akitumia kamba nyembamba ya kusafishia meno.


Inaelezwa kuwa baada ya kutoroka alitumia siku 41 kuishi msituni, akiishi kwa matunda na kuoga kwenye mito, hadi alipokamatwa tena akiwa amenyooshewa bunduki na askari baada ya kudaiwa kuiba duka la dawa karibu na mji wake wa Parkersburg.


Shepard alikuwa akikusanya kamba ndogo kwa miezi mingi zilizokuwa zinagawiwa kwa wafungwa ili kusafishia meno gerezani hapo, akaunganisha na kufuma kamba moja ndefu na imara iliyomsaidia kutoroka kupitia ukuta wa gereza wa futi 18.


Katika mahojiano yake baada ya kukamatwa Shepard alisema kua kabla ya jaribio lake kufaulu, alikuwa amejaribu kutoroka mara mbili kwa kamba hio na kushindwa kutokana na kamba kumuumiza vidole vya mikono.


Wafanyakazi watatu wa jela walifutwa kazi kwa uzembe baada ya jaribio lake la pili na lililofaulu, ambapo alitumia maelfu ya nyuzi hizo za meno ziliosokotwa hadi unene wa kamba ya wastani.

Comments

Popular posts from this blog

Mwaka 1989 Kundi Hatari la Kihalifu la Medellin Cartel la Colombia Linalomilikiwa na Pablo Escobar Lililipua Ndege na Kuuwa Abiria Wote 107, Lengo Lao Lilikuwa ni Kumuua Mgombeaji Urais wa Nchi Hiyo Álvaro Gómez

ALIKATWA MKONO, LAKINI HAIKUMZUIA KUCHEZA MPIRA KWA MAFANIKIO MAKUBWA!

Anaitwa Chris McCandless Raia wa California US. Mwaka 1992 Akiwa na Miaka 24 Aliamua Kuingia Porini, Mbali ili Akaishi Maisha ya Asili, Maisha Kama ya Wanyama kwa Miezi 3 Kisha Arudi Nyumbani. Miezi Mitatu Baadaye Mwili Wake Ulipatikana Umeoza Porini. Inaelezwa Alikufa kwa Njaa.