Anaitwa Chris McCandless Raia wa California US. Mwaka 1992 Akiwa na Miaka 24 Aliamua Kuingia Porini, Mbali ili Akaishi Maisha ya Asili, Maisha Kama ya Wanyama kwa Miezi 3 Kisha Arudi Nyumbani. Miezi Mitatu Baadaye Mwili Wake Ulipatikana Umeoza Porini. Inaelezwa Alikufa kwa Njaa.

Majina yake halisi anaitwa Christopher Johnson McCandless mzaliwa wa California US. Kwa hiyari yake mwenyewe katikati ya mwaka 1992 akiwa na miaka 24 aliamua kutoka nyumbani kwake na kuingia porini mbali huko Alaska ili kujipatia uzoefu wa maisha mapya ya asili yasiyowategemea binadamu wengine.


Chriss Aliingia porini kupata uzoefu wa kuishi maisha kama mnyama wa porini, alipanga kuishi huko kwa miezi mitatu na kurejea nyumbani huku akibeba notebook ya kuandika vidokezo pamoja na camera ndogo.


Taarifa zinasema kuwa Chris alikufa miezi mitatu baadae Agosti 18, 1992, ikiwa ni siku ya 112 baada ya kutembea porini. Mwili wake ulipatikana siku 19 baadaye pamoja na notebook yake na camera.


Kuna uwezekano mkubwa kwamba Chriss alikufa kutokana na njaa na utapiamlo. Chris alitaka kuishi kiasili akiwa porini kwa miezi michache. Kweli baada ya miezi mitatu huko porini alianza safari ya kurudi nyumbani lakini alipofika mto Teklanika alikuta mto umejaa maji mengi kiasi cha kushindwa kuvuka.


Katika wakati huo pia kutokana na ukosefu mahitaji kama chakula, alianza kudhoofu na kupungua mwili.


Katika siku zake za mwisho Chris aliandika ujumbe mfupi wa kuaga uliosomeka: “Nimekuwa na maisha ya furaha na kumshukuru Bwana. Kwaheri na Mungu awabariki wote!.” Ujumbe huu ulionyesha aliuandika katika siku ya 107.


Hata picha yake ya mwisho aliyojipiga akiwa ameshikilia ujumbe mikononi mwake katika siku ya 108 huku akiwa amvaa koti lililomzidi size kwa kukondeana, haionyeshi akijisikitikia au majuto, anatabasamu kwa amani. Inaaminika alikufa siku ya 112 kwasababu notebook haikuandikwa tena kuanzia tarehe hiyo. 


Maisha yake yamegusa mioyo ya watu wengi na amebaki kama mtu maarufu wa kuandikwa. Ni September 6 ambapo mwili wake ulikuwa umeoza huko porini .

Comments

Popular posts from this blog

Mwaka 1989 Kundi Hatari la Kihalifu la Medellin Cartel la Colombia Linalomilikiwa na Pablo Escobar Lililipua Ndege na Kuuwa Abiria Wote 107, Lengo Lao Lilikuwa ni Kumuua Mgombeaji Urais wa Nchi Hiyo Álvaro Gómez

ALIKATWA MKONO, LAKINI HAIKUMZUIA KUCHEZA MPIRA KWA MAFANIKIO MAKUBWA!