Sababu 4 Kuu Kwa Nini Iran Inasita Kuishambulia Israel Moja kwa Moja Mpaka Sasa
Kwa Nini Iran Haijaishambulia Israel Mpaka Sasa?
Hizi hapa ni sababu nne kwa nini Iran haijaishambulia Israel mpaka sasa. Kwa wale wanaojiuliza swali hili, majibu ni haya yafuatayo:
1️⃣ Hakuna Shambulio la Moja kwa Moja Kutoka Israel.
Iran haijaishambulia Israel kwa sasa kwa sababu hakuna shambulio lililotoka moja kwa moja Israel. Iran imekuwa ikishambulia nchi za Ghuba kama Bahrain, UAE, na Kuwait kwa sababu kambi za kijeshi za Marekani zilizopo katika nchi hizo ndizo zilianzisha mashambulizi dhidi ya Iran.
2️⃣ Mafundisho ya Sharia na Kanuni ya Uwiano.
Katika mafundisho ya Sharia ya Kiislamu kuhusu vita, mashambulizi hufanywa kwa uwiano na matendo ya adui anayekushambulia. Hii inamaanisha kwamba baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kuisha, ikiwa Israel ingeishambulia Iran, Iran ingejibu kwa uwiano sawa. Kulingana na misingi hii ya kivita, mashambulizi ya uchokozi (yasiyo na sababu) hayaruhusiwi. Kupigana kunaruhusiwa tu katika kujihami au kujibu uchokozi, na majibu lazima yawe ya uwiano. Hii ndiyo sababu moja wapo inayofanya Iran itangaze baadhi ya operesheni zake za kijeshi mapema ili kuonya raia, kupunguza vifo, na kuashiria kuwa malengo yake ni ya kijeshi na sio ya kiraia.
3️⃣ Kusafisha Mifumo ya Ulinzi wa Anga:
Iran inafanya kazi ya kuharibu na kusafisha mifumo yote ya ulinzi wa anga katika nchi za Ghuba, ambayo imekuwa ikizuia makombora yanayoelekezwa Israel. Pindi operesheni hii ya kusafisha mifumo ya ulinzi wa anga, hasa ile iliyopo katika jangwa la Jordan itakapokamilika, Israel itakuwa wazi kabisa na hatarini dhidi ya makombora ya balistiki ya Iran.
4️⃣ Historia Inajieleza:
Kwa wale waliosahau historia ya vita vya siku 12 na vita vya siku 39, Iran iliipiga Israel vikali sana. Kambi nyingi za kijeshi na miundombinu muhimu iliharibiwa na makombora ya balistiki ya Iran. Kuongezea, Donald Trump aliwahi kusema kwamba kama isingekuwa Marekani, Iran ingeweza kuifuta Israel.
Tusisahau kwamba nchi za Ghuba zilisaidia kuzuia mamia ya makombora ya balistiki ya Iran yaliyokuwa yakilenga Israel. Marekani pia ilipeleka mifumo ya kisasa ya ulinzi wa anga, ikiwemo THAAD, Patriot PAC-3, mifumo ya Aegis kwenye meli za kivita za Marekani yenye zana za SM-3 na SM-6, na mifumo ya rada ya AN/TPY-2 kusaidia kuzuia makombora.
Mbali na hayo, Marekani ilipeleka ndege za kivita za kisasa (kama F-15, F-16, F/A-18, F-22, na F-35) sambamba na meli za kivita katika Bahari ya Mediterania na Bahari ya Shamu. Zana hizi, zikishirikiana na mifumo ya ulinzi ya Israel ya Iron Dome, David’s Sling, na Arrow, zilicheza nafasi kubwa katika kuzuia makombora na ndege zisizo na rubani (drones) za Iran.
Kwa wale wanaosema Iran haiwezi kuthubutu kuishambulia Israel, aidha hawajui historia au wanazungumza kutokana na ushabiki wa kuunga mkono Israel.
Iran ina akiba kubwa mno ya makombora. Lakini anayesema Iran inaweza kuipiga Israel kirahisi anapuuza ukuta mkubwa wa kiteknolojia uliowekwa. Umoja wa kijeshi kati ya mifumo ya Marekani (THAAD, Patriot, Aegis) na ile ya Israel (Iron Dome, Arrow, David's Sling) umetengeneza mwavuli mgumu sana wa chuma angani ambao ni mgumu sana kupenyeka. Hii ndiyo maana halisi ya vita vya kisasa sio ushirikina au miujiza, bali ni sayansi, teknolojia na ushirikiano wa kijeshi.
@Swahili Prime Ent
Comments
Post a Comment