Mwaka 1989 Kundi Hatari la Kihalifu la Medellin Cartel la Colombia Linalomilikiwa na Pablo Escobar Lililipua Ndege na Kuuwa Abiria Wote 107, Lengo Lao Lilikuwa ni Kumuua Mgombeaji Urais wa Nchi Hiyo Álvaro Gómez
Mei 27, 1990 ulifanyika uchaguzi mkuu nchini Colombia huku wagombea urais wakiwa ni César Gaviria wa chama cha Liberal na mpinzani wake Álvaro Gómez Hurtado wa chama cha MSN, Cesar alipita kwa asilimia 48% za kura na kuwa rais wa 28 wa Colombia.
Katika kampeni zilizoanza tangu mwaka 1989, mgombea Alvaro alikuwa akitumia sera ya kutokomeza biashara ya dawa za kulevya nchini humo akidai kuwa serikali ya awamu iliyopita imekuwa ikishirikiana na makundi makubwa ya dawa za kulevya hivyo yeye akichaguliwa kuwa rais atakomesha biashara hiyo haramu.
Moja ya makundi hatari ya biashara hio nchini humo ni Medellin Cartel linalomilikiwa na mtu m'bad Pablo Escobar, walivyosikia ngebe hizo mipango ya kutoa uhai wa mgombea huyo ikaanza.
Taarifa zilizowafikia wauza unga hao ni kwamba Alvaro alitarajia kusafiri siku ya November 27, 1989 kutoka Bogotá kwenda Soacha kwa usafiri wa ndege ya shirika la ndege la Boeing 727, Avianca Flight 203, ndipo walipanga kuilipua ndege hiyo ili kumteketeza mgombea huyo wa Urais.
Ni kweli jumatatu ya November 27, 1989, majira ya saa 07:18 asubuhi saa za Colombia, ndege ya Avianca Flight 203 ililipuka dakika chache baada ya kupaa na kuuwa watu wote 107 waliokuwamo katika ndege hiyo.
Lengo la ulipuzi huo ilikuwa ni kumuua mgombea wa urais Alvaro kutokana na sera zake za kupiga vita dawa za kulevya, lakini bahati mbaya kwao ni kwamba Alvaro hakuwemo katika ndege hiyo, na alifanikiwa kuwamo katika uchaguzi wa Mei 1990 japo alianguka vibaya kwa kupata asilimia 28 tuu ya kura zote.
Licha ya Alvaro kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 1990, lakini pia aligombea katika uchaguzi uliopita wa mwaka 1986 na sera zake zikiwa ni hizo hizo za kutokomeza biashara ya dawa za kulevya, sera zilizokuwa mwiba kwa wahusika wa biashara hiyo.
Hata hivyo Alvaro Gómez Hurtado aliuwawa kwa kupigwa risasi miaka kadhaa baadae November 2, 1995 huko Bogotá. Alishawahi kutekwa mara kadhaa pia miaka ya 1988.
Uchunguzi wa ajari hiyo mbaya ulibaini kuwa kuna bomu lilitegwa chini ya siti kabla ya dege kuruka na kusababisha hasara hiyo kubwa ya mali pamoja na watu. Hata hivyo baadaye mtegaji wa bomu alifahamika na kukamatwa, anaitwa Dandeny Munoz-Mosquera mwenye umri wa miaka 56 sasa.
Dandeny ambaye ni mzaliwa wa Medellín Colombia alikuwa ni mmoja wa wanakikundi wa uuzaji wa dawa za kulevya wa Medellin Cartel, mwaka 1991 alihukumiwa vifungo 10 vya maisha pamoja na miaka 45 jela kwa pamoja.
Swahili Prime Ent:
Comments
Post a Comment